
Jinsi ya kufanya ukitaka kutumia Yai kuboresha muonekano wa ngozi na nywele zako.
Chukua Yai, changanya na asali kijiko kimoja cha chai mafuta ya Olive .Chukua mchanganyiko huo kisha pakaa usoni na shingoni, kaa nao kwa dakika kumi hadi 15. Hii itasaidia kama una mashimo usoni yatokanayo na chunusi kubana.
Pia itasaidia kulainisha ngozi yako na kuwa nyororo, mchanganyiko huu pia utasaidia kukuondolea michubuko au alama za kuungua na jua, mafuta au krimu usoni.Unaweza kutenganisha kiini cha Yai na ule ute mweupe, kisha chukua ute weka kwenye kikombe au bakuli, baada ya hapo pigapiga ule ute hadi uwe na mapovu kisha chukua povu, linawe usoni au paka mwili mzima kisha liache likauke .

Iwapo unasumbuliwa na kuwashwa ngozi, matumizi ya Yai pia ni njia sahihi kuepuka tatizo. Maski ya Yai ina utajiri wa ‘Acid’ za Amino ambazo husaidia kupunguza na kuondoa miunguzo au muwasho mwilini kutokana na protini inayopatikana kwenye Yai.
Kama unawashwa mwili mzima, chukua ute wa yai kidogo halafu nyunyiza katika maji utakayoyaoga sambamba na sabuni ya kuogea ndani ya siku chache utaona matokeo.

Kwa upande wa nywele wale ambao, nywele zao hazina afya au ukuaji wao ni hafifu wanaweza kupaka yai kichwani, hakikisha inagusa mizizi inayosaidia kuotesha nywele, kama nilivyoeleza awali protini iliyopo kwenye yai ndio chanzo cha kila kitu.Unaweza kutumia Yai kama ‘Hair Conditioner’, chukua kiini chake changanya na asali, mafuta ya watoto na maji kidogo.
Changanya vizuri kisha paka kichwa kizima acha kwa dakika 20 kisha osha na maji ya baridi chukua ute mweupe changanya na shampoo yako kidogo
No comments:
Post a Comment