Popular Posts

Saturday, October 22, 2011

UREMBO WA KUCHA


  Hizi kucha ni nzuri sana tena sana sana kwa maharusi maana wanakuwa hawana haja ya kuvaa gloves .

Monday, October 10, 2011

YAI KWA UREMBO WA NGOZI NA NYWELE....................

Urembo:Yai kwa urembo wa ngozi, nywele
 
YAI limekuwa na matumizi kama chakula kwa muda mrefu, wapo ambao hutumia chakula hicho kwa kukaanga, kuchemsha, kunywa likiwa bichi na au kuchanganya katika vyakula vingine mbalimbali.Lakini pia kuna matumizi ya Yai zaidi ya chakula, kwani linauwezo mkubwa wa kurutubisha ngozi,  nywele na pia kuondoa uchovu.
Jinsi ya kufanya ukitaka kutumia Yai kuboresha muonekano wa ngozi na nywele zako.
Chukua Yai, changanya na asali kijiko kimoja cha chai  mafuta ya Olive .Chukua mchanganyiko huo kisha pakaa usoni na shingoni, kaa nao kwa dakika kumi hadi 15. Hii itasaidia kama una mashimo usoni yatokanayo na chunusi kubana.

Pia itasaidia kulainisha ngozi yako na kuwa nyororo, mchanganyiko huu pia utasaidia kukuondolea michubuko au alama za kuungua na jua, mafuta au krimu usoni.Unaweza kutenganisha kiini cha Yai na ule ute mweupe, kisha chukua ute weka kwenye kikombe au bakuli, baada ya  hapo pigapiga ule ute  hadi uwe na mapovu kisha chukua povu,  linawe usoni au paka mwili mzima kisha liache likauke .
 Baada ya hapo osha na maji ya uvuguvugu, ukifanya hivyo mara kwa mara itakusaidia kufanya ngozi yako iwe anga’avu.Kama umetoka kazini na unaonekana umechoka na unataka kutoka usiku, chukua ute wa yai na pakaa chini ya jicho na uache kwa dakika 10 hadi 15 kisha safisha, itasaidia kuondoa muonekano wa uchovu katika macho yako.
Iwapo unasumbuliwa na kuwashwa ngozi, matumizi ya Yai pia ni njia sahihi kuepuka tatizo. Maski ya Yai ina utajiri wa ‘Acid’ za Amino ambazo husaidia kupunguza na kuondoa miunguzo au muwasho mwilini kutokana na protini inayopatikana kwenye Yai.
Kama unawashwa mwili mzima,  chukua ute wa yai kidogo halafu nyunyiza katika maji utakayoyaoga sambamba na sabuni ya kuogea ndani ya siku chache utaona matokeo.




Kwa upande wa nywele wale ambao, nywele zao hazina afya au ukuaji wao ni hafifu wanaweza kupaka yai kichwani, hakikisha inagusa  mizizi inayosaidia kuotesha nywele, kama nilivyoeleza awali protini iliyopo kwenye yai ndio chanzo cha kila kitu.Unaweza kutumia Yai kama ‘Hair Conditioner’, chukua kiini chake changanya  na asali, mafuta ya watoto na maji kidogo.


Changanya  vizuri kisha paka kichwa kizima acha kwa dakika 20 kisha osha na maji ya baridi chukua ute mweupe changanya  na shampoo yako kidogo

Saturday, October 8, 2011

MITINDO MBALIMBALI......

Natumaini tunaendelea vizuri na kazi za ujenzi wa taifa na kwahilo nawashukuru wote kwakuwa Taifa lolote ujengwa na wananchi wenyewe kwa kufanya kazi kwa bidii.....
    Leo ningependa tutazame aina tofauti za magauni(dressing style).... tazama hapo chini...


1.ametoka bomba......kama umeipenda nambie!
 
2.muangalie na huyu pia......                                 3. na huyu ametoka

4.ametoka sana....                                      5.wooow.......
 
 

ONGEZA UREMBO.........

Ogoza urembo wa ngozi kwa kutumia chumvi
PAMOJA na kutumiwa  kama kiungo  katika mapishi mbalimbali. Chumvi ina umuhimu wake katika suala zima la urembo.
 
Je, unafahamu kuwa chumvi inaweza kutumika kama kipodozi na kukuacha ukiwa na ngozi nyororo na ya kuvutia?
 
Kumekuwepo na sababu mbalimbali zinazopelekea warembo kupata matatizo ya ngozi. Kitendo hicho huwafanya warembo husika kupoteza nuru ya ngozi zao na pia matumaini ya kuonekana wenye kuvutia na kupendeza.
Matatizo ya chunusi, ukavu katika ngozi, mafuta usoni na hata mlundikano wa ngozi zilizokufa usoni ni miongoni mwa mambo yanayowakera warembo wengi na hatimaye kupelekea kutumia vipodozi visivyo salama kwa ngozi zao.
 Kwa kutambua hilo wataalamu wa urembo wa asili walikuja na njia hii ambayo haina gharama kubwa ukilinganisha na njia zilizozoeleka na warembo wengi.
 Matumizi ya chumvi yamekuwa na matokeo mazuri katika matatizo mbalimbali ya ngozi, ingawaje si wengi wanalolifahamu hili.
Unachotakiwa kuzingatia ni kuhakikisha kuwa chumvi hiyo haingii machoni mara utakapoanza kuitumia.
Mahitaji.
 
Chumvi ya unga kijiko 1 kikubwaNamna ya kufanya
 Nawa uso wako kwa maji ya kawaida na kisha chukua kitambaa laini na safi. Chovya kwenye chumvi na kisha sugua katika ngozi yako ya uso taratibu.
Baada ya kupaka katika uso mzima, weka chini kitambaa chako na kisha jisugue kwa kutumia mikono yako. Fanya hivyo hadi utakapoona takataka zinatoka. 
 
Baada ya kufanya hivyo kwa muda wa dakika mbili, osha kwa kutumia maji ya baridi.
Ni muhimu kufanya zoezi hili mara kwa mara kwani bila hivyo krim au losheni yako unayotumia haitafika katika ngozi pindi unapotaka kufanya hiyo.
 
Unashauriwa kufanya aina hii ya scrub mara moja kwa wiki ili kupata matokeo mazuri.
Imeandaliwa na Maimuna Kubegeya

KARIBU TUJUMIKE pamoja.........

........Natumaini hu mzima wa afya,mi nashukuru kwakuwa umepata muda wa kujumuika nami katika blod hii....nimesukumwa na moyo wangu mimi mwenyewe kuanzisha blog hii ili niweze kuelezana na wanawake wenzangu mambo mengi kuhusu UREMBO....Karibu tuwe pamoja.....