PAMOJA na kutumiwa kama kiungo katika mapishi mbalimbali. Chumvi ina umuhimu wake katika suala zima la urembo.
Je, unafahamu kuwa chumvi inaweza kutumika kama kipodozi na kukuacha ukiwa na ngozi nyororo na ya kuvutia?
Kumekuwepo
na sababu mbalimbali zinazopelekea warembo kupata matatizo ya ngozi.
Kitendo hicho huwafanya warembo husika kupoteza nuru ya ngozi zao na pia
matumaini ya kuonekana wenye kuvutia na kupendeza.
Matatizo
ya chunusi, ukavu katika ngozi, mafuta usoni na hata mlundikano wa ngozi
zilizokufa usoni ni miongoni mwa mambo yanayowakera warembo wengi na
hatimaye kupelekea kutumia vipodozi visivyo salama kwa ngozi zao.
Kwa
kutambua hilo wataalamu wa urembo wa asili walikuja na njia hii ambayo
haina gharama kubwa ukilinganisha na njia zilizozoeleka na warembo
wengi.
Matumizi ya chumvi yamekuwa na matokeo mazuri katika matatizo mbalimbali ya ngozi, ingawaje si wengi wanalolifahamu hili.
Unachotakiwa kuzingatia ni kuhakikisha kuwa chumvi hiyo haingii machoni mara utakapoanza kuitumia.
Mahitaji.
Chumvi ya unga kijiko 1 kikubwaNamna ya kufanya
Nawa
uso wako kwa maji ya kawaida na kisha chukua kitambaa laini na safi.
Chovya kwenye chumvi na kisha sugua katika ngozi yako ya uso taratibu.
Baada
ya kupaka katika uso mzima, weka chini kitambaa chako na kisha jisugue
kwa kutumia mikono yako. Fanya hivyo hadi utakapoona takataka zinatoka.
Baada ya kufanya hivyo kwa muda wa dakika mbili, osha kwa kutumia maji ya baridi.
Ni
muhimu kufanya zoezi hili mara kwa mara kwani bila hivyo krim au
losheni yako unayotumia haitafika katika ngozi pindi unapotaka kufanya
hiyo.
Unashauriwa kufanya aina hii ya scrub mara moja kwa wiki ili kupata matokeo mazuri.
Imeandaliwa na Maimuna Kubegeya
|
HI nimenufaika
ReplyDeleteila hapa kuna yongeza kwa yoyote
ReplyDeleteanayependa kujipatia fedha huku akipendeza
ingia kwenye link hii wengi wamenufaika http://4ui.us/ingiahapa